UFUNGUZI WA KONSELI YA HESHIMA TORONTO, CANADA
Posted by Unknown on 1:02:00 AM
Mhe. Jack Mugendi Zoka, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania nchini Canada akimkaribisha Konseli wa Heshima Mteule, Bw.
Deepak Ruparell kwenye chumba cha wageni cha Ubalozi mara baada ya
kuwasili.Tarehe 29 Aprili, 2016 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ilitiliana saini mkataba wa kufungua Ofisi ya Konseli ya
heshima jijini Toronto, Canada. Mkataba huo ulitiwa saini kati ya
Konseli wa Heshima, Bw. Deepak Ruparell na Mhe. Jack Mugendi Zoka Balozi
wa Tanzania Nchini Canada ambaye aliiwakilisha Serikali ya Tanzania.
Tukio hilo lilifanyika kwenye ofisi za Ubalozi wa Tanzania zilizopo
jijini Ottawa nchini Canada