Israel yazindua Kituo cha Kutoa VIZA
Posted by Unknown on 12:42:00 AM
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Prof. Jumanne Maghembe (Mb) ambaye alikuwa Mgeni Rasmi kwenye sherehe za kufungua Kituo cha Kutoa viza za kwenda nchini Israel akiwasilisha hotuba katika ufunguzi huo. Prof. Maghembe alipongeza uamuzi wa Israel kufungua kituo hicho hapa nchini kwa kuwa kitarahisisha ziara za kwenda Israel kwa Watanzania. Aidha, alirejea kauli ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu dhamira ya Serikali ya kufungua Ubalozi nchini Israel. Prof. Maghembe alieleza kuwa idadi ya watalii kutoka Israel kuja Tanzania inaendelea kuongezeka na jana alikutana na wakala wa usafirishaji kutoka nchi hiyo ambao wana nia ya kuanza safari za ndege za kila wiki kutoka Israel hadi mkoani Katavi (charter flights) kutembelea maoeneo ya utalii. Ndege aina kama hiyo inafanya safari za kuja Tanzania katika mikoa ya kaskazini mara mbili kwa mwaka. Prof. Maghembe alisisitiza umuhimu wa Tanzania kushirikiana na Israel katika sekta ya teknolojia hususan mbinu za kitaalamu za kukabiliana na ujangili wa wanayamapori nchini.Kituo cha viza kitakuwa na ofisi za muda kwenye Hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.