Balozi wa Tanzania nchini Kuwait akutana na Balozi wa Chad nchini humo.

Posted by Unknown on 3:12:00 AM
Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim, Balozi wa Tanzania nchini Kuwait akizungumza na Mhe. Ali Ahmed Aghabache, Balozi wa Chad nchini Kuwait alipomtembelea Ofisini kwake hivi karibuni. Katika mazungumzo yao Mhe. Maalim alimweleza Balozi Aghabache kuhusu ushiriki wa Tanzania katika maadhimisho ya Siku ya Afrika ambayo huadhimishwa tarehe 25 Mei ya kila mwaka. Chad ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) kuanzia Januari 2016.

 Maadhimisho ya Siku ya Afrika huvuta hadhira ya viongozi mbalimbali wa Serikali, waandishi wa habari, mifuko ya fedha na uwekezaji na taasisi zinazojihusisha na masuala ya kibinadamu na hutumiwa na Mabalozi wa nchi za Afrika waliopo Kuwait  kama jukwaa la kutangaza fursa  za uwekezaji, biashara na vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo.