MAKAMU WA RAIS AWASILI NCHINI PAPUA NEW GUINEA KUMUWAKILISHA RAIS MAGUFULI KATIKA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA
Posted by Unknown on 12:38:00 AM
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Belize Bw. Wilfered
Eliringron wakati Makamu wa Rais alipowasili katika Hoteli ya Airways
mjini Papua New Guinea.
Makamu wa Rais yupo Nchini Papur New Guinea kwa
ajili ya kumwakilisha Rais John Magufuli katika mkutano wa siku mbili
unaotarajiwa kuanza kesho utakaojadili masuala ya kukuza Usawa na
Maendeleo endelevu kwa ajili ya Wananchi wa Nchi wanachama kuimarisha
majukumu ya Nchi za ACP katika Utawala Bora na Maendeleo, Usalama na
Utulivu wa kisiasa. Mkutano huo utahudhuriwa na Wakuu wa Nchi za
Afrika, Caribbean na Pacific (ACP).