Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim, Balozi wa Tanzania nchini
Kuwait akiwa katika mazungumzo na Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya
Nje ya Kuwait, Mhe. Balozi Dhari Ajran Al-Ajran alipomtembelea Ofisini
kwake kwa ajili ya kumshukuru kwa mchango wake binafsi pamoja na Wizara
ya Mambo ya Nje ya Kuwait katika kufanikisha juhudi za Tanzania kufungua
Ubalozi wake nchini humo. Kadhalika, Mhe. Maalim alimuhakikishia Mhe.
Al-Ajran utayari wa Tanzania katika kuhakikisha mahusiano baina yake na
Kuwait katika nyanja za kisiasa, kiuchumi na kijamii yanasonga mbele
zaidi.